Na Mwandishi Wetu
Mashirika yasiyo ya kiserikali wilayani Kasulu mkoani Kigoma yamehimizwa kushirikiana na serikali katika kuhakikisha suala la lishe bora linazingatiwa mashuleni.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kasulu, Theresia Mtelewe aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe. Kanali Isaac Mwakisu ametoa wito huo leo Jumanne Julai 16, 2024 wakati wa Kikao cha Taasisi Zisizo za Serikali kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu.
“Tumeendelea kujikita katika masuala ya afya na lishe mashuleni wakati mwingine tunapata ukinzani kutoka kwa wazazi kwakuwa ni kitu kipya… nyinyi mpo mshirikiane na serikali kwa kutembelea hizi ofisi kuona ni namna gani mnaweza kuwashawishi watoto wetu waendelee kupata lishe bora,” amesema.
Aidha, ameyataka mashirika hayo kutoa taarifa sahihi kwa serikali pale zinapohitajika na kusisitiza miradi wanayotegemea kuitekeleza ifanyike sehemu zenye mahitaji, malengo na vipaumbele vya taifa.
Na kuongeza kuwa serikali haitosita kuchukua hatua kwa taasisi ambayo itakuwa inafanya mambo ambayo hayaendani na mila, tamaduni na desturi za mtanzania.
Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Kasulu, Elimiliki Kihundrwa ametoa wito kwa taasisi hizo kupeleka habari kwa jamii kuacha kushusha thamani ya utu wao kwa kuwaomba wagombea rushwa.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.