Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya Awamu ya Sita itaendelea kumuenzi aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati John Magufuli kwa kusimamia na kuyandeleza mazuri yote aliyoyaanzisha.
Rais Samia ameyabainisha hayo leo Jumapili Machi 17, 2024 kupitia akaunti yake ya Twitter zikiwa ni salamu zake katika kumbukizi ya miaka mitatu ya kifo cha Hayati Magufuli.
"Tarehe kama ya leo miaka mitatu iliyopita tuliondokewa na aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dk John Pombe Magufuli. Tuendelee kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ampe pumziko jema," amesema Samia.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.