Imeelezwa kuwa Mfumo wa Manunuzi wa Umma (NeST) ulianzishwa ili kusaidia kudhibiti kuchelewa na kuongeza uwazi wakati wa mchakato wa zabuni.
Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Manunuzi ya Umma (PPRA) Kanda ya Kati, Mhandisi Suma Atupele ameyasema hayo leo alipokutana na wakuu wa idara, vitengo na watendaji wa Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi na Ugavi wa Halmshauri ya Wilaya ya Kasulu.
Ambapo amewataka wakuu wa idara na vitengo pamoja na watu walio chini yao kuhakikisha mchakato wa manunuzi wanaufanya wao wenyewe na kukemea tabia ya utoaji wa nywila ili waweze kufanyiwa shughuli hizo.
“Hii mifumo ni mipya maadamu umepewa akaunti useme sijuhi uelekezwe utajua taratibu na si kumuachia nywila yako mtu anayehusika na manunuzi,” amesema.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Magdalena Segeja amesema kuwa utendaji kazi serikalini unapoelekea itafika kipindi matumizi ya karatasi yatafikia kikomo na kuwataka wakuu wa idara na vitengo kutilia mkazo suala la kufahamu mifumo.
Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi na Ugavi, Gwamaka Panja amebainisha changamoto ya mfumo kutotambua baadhi ya wazabuni wanapotangaza kazi.
Kwa upande wake Afisa Ugavi na Ununuzi, Ezekiel Badeleya amesema kuwa mfumo huo umeongeza uwazi na uwajibikaji lakini halmashauri uwa inakwama inapotaka kuuza au kukodisha kitu.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.