Na. Andrew Ginnethon-Kasulu
Mvua kali zinazoendelea kunyesha katika wilaya ya Kasulu na Mkoa wa Kigoma kwa ujumla, zimepelekea kifo cha Mtu mmoja wilayani hapa.
Tukio hilo limetokea siku ya Jumamosi Tarehe 30.3.2019 katika kijiji cha Muzye kilichopo kata ya Muzye, ambapo mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Steria Bilega(72) mkazi wa Kitongoji cha Migogwe, alisombwa na maji na kupelekea Kifo chake wakati akivuka korongo lililokuwa linapitisha maji wakati akitoka shambani.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Muzye Ngd. Edward Guruza, amesema kuwa tukio hilo limetokea muda wa Saa tano , ambapo marehemu akiwa ameambatana na wajuu zake wawili, alikutwa na umauti baada ya kuteleza na kutumbukia kwenye korongo lililokuwa linapitisha maji kwa kasi wakati mvua inanyesha.
Aidha Mwenyekiti wa Kitongoji cha Migogwe ambapo marehemu alikuwa akiishi Ndg. Charles Badili, amesema kuwa wajukuu wa Marehemu ndio waliotoa taarifa ya tukio, kisha wakazi wa kitongoji hicho waliamua kwenda kufuatilia na kuukuta mwili wa marehemu ukiwa umbali wa takribani zaidi ya Mita Hamsini kutoka kwenye korongo alikoteleza na kusombwa na Maji.
Ndg. Moses Mloka ambaye ni mkazi wa kitongoji hicho, amesema baada ya kufuatilia waliukuta mwili wa marehemu ukiwa umefukiwa na mchanga huku kichwa na sehemu ya mkono vikiwa nje. Amesema kwa kushirikiana na wanakitongoji, walifanikiwa kuuchukua mwili huo kisha kuurejesha kijijini tayari kwa taratibu za mazishi.
Diwani wa Kata hiyo, Mh Said Ndiyunze amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kushauri wakazi wa kata ya Muzye na maeneo ya jirani, kuwa makini kuvuka katika maeneo yanayopitisha maji hususani kipindi hiki cha Mvua kali.
“Wananchi wanategemea Kilimo na nyakati hizi zinaponyesha, a ni vema wakasubiri maji yapungue ndipo wavuke kwenye mito wanapoenda au kurejea kutoka mashambani” alihitimisha Ndiyunze.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.