Na Mwandishi Wetu Kasulu
Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Dkt. Semistatus H. Mashimba leo Jumatatu Oktoba 21,2024 amefanya mkutano na waandishi wa habari ambapo kupitia tukio hilo ametaja mambo manne ambayo halmashauri iliyafanya hadi kufanikisha zoezi la kuandikisha wapiga kura kwenye Daftari la Mkazi.
Dkt. Mashimba amesema kitu cha kwanza kilichosaidia zoezi hilo kufanikiwa ni kuzingatia maelekezo ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan yanayotaka utumikaji wa 4R zake katika shughuli zote kubwa za kitaifa zinazoakisi maridhiano, mabadiliko, ustahimilivu na kujenga upya.
-
“Kupitia misingi hiyo katika zoezi la mchakato mzima wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa pamoja na uandikishaji katika wilaya yetu tulishirikiana na viongozi wote wa chama na serikali,vyama vyote vya siasa, makundi ya wazee maarufu, vijana na vikundi vya sanaa ili kuhakikisha zoezi linafanikiwa,” amesema.
Pia, amesema kuwa suala la kuzingatia miongozo waliyopewa na viongozi mbalimbali kuanzia ngazi ya mkoa,wilaya pamoja na halamshauri nayo imekuwa sababu mojawapo ya kukamilisha mchakato vizuri.
Aidha, amesema kuwa kitu kingine kilicho fanikisha zoezi hilo ni miongozo na kanuni iliyoratibiwa vizuri na Waziri wa OR Tamisemi, Mhe. Mohamed Mchengengerwa ambayo imesaidia vifaa na fedha kufika kwa wakati na kupelekea mchakato kutokuwa na dosari.
Katika hatua nyingine Dkt. Mashimba amewashukuru waandishi wa habari wilayani Kasulu kwa hamasa kubwa waliyoitoa na kupekea watu kwenda kujiandiskisha na ndio maana hatua moja hadi nyingine ya uchaguzi huo zimekwenda vizuri.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.