• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe ya Ofisi |
Kasulu District Council
Kasulu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Kilimo-Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
    • Muundo wa Utawala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Elimu
    • Afya
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Utawala na Mipango
      • UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
      • MRADI WA UMWAGILIAJI TITYE
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogondogo
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu za Maombi
    • Taratibu
    • Huduma Kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Makala
    • Matangazo

MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2018 KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA KASULU.

Posted on: April 18th, 2018

Na.Andrew Mlama.

Mwenge wa Uhuru umekamilisha ziara yake katika Halmashauri ya Kasulu baada ya kupita kwenye Miradi inayotekelezwa yenye jumla ya Thamani ya shilingi ya Tshs. 1,919,836,028/=. Katika Miradi hiyo  Serikali Kuu imechangia Tshs. 937,869,500/= sawa na asilimia 49, Michango ya Wananchi ni Tshs. 96,160,592/= sawa na asilimia 5 na Wadau wa Maendeleo wamechangia Tshs. 885,805,936/= sawa na asilimia 46.

Mbio hizo zimefanyika leo tarehe 18/04/2018 ambapo umefanyika uzinduzi wa Mradi wa ujenzi wa wodi ya wazazi Zahanati ya Makere, Mradi wa maji Nyamidaho, Ujenzi wa Bwalo la chakula shule ya Sekondari Muyovozi, Skimu ya umwagiliaji Rungwempya na klabu ya kupinga na kupambana na Rushwa shule ya Sekondari Titye. Aidha umefanyika uwekaji jiwe la msingi Kituo cha Afya Nyakitonto na kufungua nyumba tano za watumishi katika Kituo cha Afya Shunga,

Mwenge wa Uhuru umepokelewa katika Kata ya Nyamidaho Wilayani hapa, ambapo katika hotuba yake, Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa Ndg. Charles Francis Kabeho alisema kuwa umati wa watu waliojitokeza kuupokea Mwenge wa Uhuru ni ishara tosha kuwa Kasulu kuna amani, upendo na mshikamano.

Akihutubia wakazi waliojitokeza kwa wingi katika eneo la mapokezi ya Mwenge wa Uhuru, Amempongeza Rais wa Serikali ya awamu ya tano Dkt. John Pombe Magufuli  kwa kuhakikisha Elimu ya Msingi mpaka Sekondari inatolewa bure “Serikali ilizuia michango katika shule zake hivyo mwalimu Mkuu au Kamati ya shule wasichangishe Michango bali ichangishwe na Kamati ya Maendeleo ya kata au vijiji kwa kufuata muongozo unaopatikana kwa Mkurugenzi’’alisema Kabeho.

Amesema Mkoa wa Kigoma haupo katika orodha ya Mikoa yenye utoro sugu. Amewataka wazazi kufuatilia mahudhurio na maendeleo ya kitaaluma ya watoto wao shuleni. Aidha amesisitiza jumkumu la wazazi kuhakikisha wananunua Sare za Shule za watoto  wao kwani kutofanya hivyo ni kutotekeleza wajibu na majukumu yao.

Amewataka wananchi  kuongeza kasi ya mapambano dhidi ya rushwa, matumizi ya madawa ya kulevya,kupambana na kudhibiti UKIMWI pamoja na malaria.

Akisoma risala ya utii kwa niaba ya Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Katibu Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu ndg. Mguha T.Mguha alifafanua kuwa Wananchi wa Kasulu wametekeleza ujumbe wa Mwenge wa Uhuru mwaka 2018 kwa kujenga shule za Sekondari, kutoa elimu ya kujikinga dhidi ya VVU/UKIMWI, kusaidia mapambano dhidi ya malaria, kutoa elimu ya Mapambano dhidi ya rushwa na kupiga vita madawa ya kulevya.

“Kwa niaba ya Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu tunawashukuru Wakimbiza Mwenge Kitaifa, Kimkoa na Kiwilaya, Viongozi wa ngazi ya Mkoa na Wananchi wote kwa ujumla, kwa jinsi tulivyoshirikiana na kufanikisha Mbio za Mwenge wa Uhuru hapa Wilayani kwetu Kasulu’’ alihitimisha Mguha.

 Mwenge wa Uhuru utaendelea na ziara yake katika Halmashauri ya mji wa Kasulu.

Matangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO ILIYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU January 08, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI February 17, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA February 21, 2024
  • MWALIKO WA ZABUNI KUPANGISHA ENEO KWAAJILI YA MGAHAWA March 08, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • PAMBA KUINUA UCHUMI WA WAKULIMA

    May 08, 2025
  • WASHIRIKI WA MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA WAHASWA KUFANYA KAZI KWA BIDII

    April 29, 2025
  • MAWAKALA WA VYAMA KURUHUSIWA KITUONI KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA

    April 29, 2025
  • MAWAKALA WA VYAMA KURUHUSIWA KITUONI KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA

    April 29, 2025
  • Angalia Zote

Video

NAIBU WAZIRI OR-UTUMISHI NOV 2022
Video zaidi

KURASA ZA KARIBU

  • PlanRep_Web_Based
  • FFARS Online Manual
  • PlanRep Online Manual
  • Facility Financial Accounting and Reporting System (FFARS)
  • safari_Live
  • safaridemo
  • Dashibodi ya Ukusanyaji wa Mapato
  • UNICEF Dashboard
  • Kamusi Eng & Swa

TOVUTI ZINAZOHUSIANA

  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • TAMISEMI
  • BUNGE
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • ARIDHI
  • OPEN UNIVERSITY
  • PSPTB
  • AJIRA
  • HFR Dashboard
  • KIGOMA DC
  • NACTE
  • NECTA
  • eMrejesho

Kihesabu watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU

    Anuani ya Posta: S.L.P 97

    Simu ya Mezani: +255-028-2810339

    Simu: +255-028-2810339

    Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera Ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma
    • Wasiliana Nasi

Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.