Na Mwandishi Wetu
Imeelezwa kuwa ili kuleta uwazi katika zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mawakala wa vyama vya siasa wataruhusiwa kuwepo katika vituo vya kuandikisha wapiga kura.
Hayo yamebainishwa jana Julai 17,2024 na Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Kasulu Vijijini, Emmanuel Ladislaus wakati akifungua Semina ya Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa Waandishi Wasaidizi na Waendesha Vifaa vya Bayometriki.
“Mawakala wa vyama vya siasa wataruhusiwa kuwepo katika vituo vya kuandikisha wapiga kura, jambo hili ni muhimu kwa kuwa linaleta uwazi katika zoezi zima pia mawakala hao watasaidia kutambua wapiga kura wa eneo husika,” amesema.
Aidha, amewataka washiriki wa mafunzo hayo kuhakikisha wanavitunza vifaaa vyote watakavyokabidhiwa kwa kuzingatia maelekezo yatakayotolewa na Afisa Mwandikishaji na wasaidizi wake ili yaweze kufanyiwa kazi pindi zoezi litakapoanza.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.