Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Dkt. Semistatus H. Mashimba mapema leo Ijumaa amekutana na watendaji wa vitengo vya Habari na Mawasiliano Serikalini pamoja na TEHAMA wa halmshauri hiyo.
Katika kikao hicho Mashimba ameonesha kufurahishwa kwa namna vitengo hivyo vinavyoshirikiana katika kutangaza shughuli mbalimbali zinazofanywa na serikali wilayani humo.
“Nawapongeza kwa namna mnavyohuisha taarifa kwenye tovuti na mitandao yetu ya kijamii hivyo nawasisitiza kasi mliyokuwa nayo muindeleze zaidi,” amesema.
Pia, ametaka vitengo hivyo kushirikishwa katika shughuli mbalimbali za viongozi na wananchi ili kubainisha kazi kubwa inayofanywa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na kuibua mahitaji muhimu ya wananchi.
Katika hatua nyingine Mashimba ameagiza ufungwaji wa kamera za usalama za kisasa katika ofisi za halmashauri ili kuboresha usalama katika maeneo hayo.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.