Miongoni mwa miradi ya ujenzi inayofanyika na kutekelezwa kwa ufanisi na umaridadi mkubwa katika miradi ya ujenzi iliyopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, ni ujenzi wa wodi tatu za wagonjwa zinazojengwa kwenye hospitali ya halmashauri hiyo.
Ujenzi wa wodi hizo uliokuwa umekadiriwa kukamilika kwa gharama ya shilingi milioni 500, unahitaji nyongeza ya shilingi milioni 105 ongezeko linalotokana na kupanda kwa gharama za ujenzi na uzingatifu wa ubora na viwango katika ujenzi wa wodi hizo.
Kutokana na hali hiyo, haikuwa vigumu kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI) mheshimiwa Ummy Mwalimu kutoa ahadi ya kuongezea pesa hizo ili kukamilisha ujenzi wa wodi hizo wakati alipokuwa kwenye ziara yake Julai mwaka huu.
Pichani ni muonekano wa sehemu ya wodi hizo katika sura tofauti.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.