• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe ya Ofisi |
Kasulu District Council
Kasulu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Kilimo-Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
    • Muundo wa Utawala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Elimu
    • Afya
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Utawala na Mipango
      • UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
      • MRADI WA UMWAGILIAJI TITYE
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogondogo
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu za Maombi
    • Taratibu
    • Huduma Kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Makala
    • Matangazo

MAFUNZO YA SIKU TATU YA KKK KWA WALIMU WA DARASA LA KWANZA NA LA PILI YAFIKIA TAMATI KASULU

Posted on: June 5th, 2025

Na Mwandishi Wetu 

Mafunzo ya siku tatu kuhusu kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK) kwa walimu wa darasa la kwanza na la pili kutoka shule 88 zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, mkoani Kigoma, kupitia Mradi wa Shule Bora, yamehitimishwa rasmi leo.

Katika mafunzo hayo, washiriki wamehimizwa kutumia maarifa waliyojifunza kuboresha ufundishaji kwa kutumia zana mbalimbali, kwa kuwa mbinu hizo husaidia wanafunzi wa madarasa ya awali kuelewa haraka na kwa ufanisi zaidi.

Akifunga rasmi mafunzo hayo katika Chuo cha Ualimu Kabanga, Afisa Elimu Taaluma (Msingi) wa halmashauri hiyo,  Joseph Maiga, amewataka walimu kuhakikisha wanayatekeleza kwa vitendo yale yote waliyojifunza, ili mabadiliko katika ufundishaji wa KKK yaonekane wazi katika vituo vyao vya kazi.

“Kutakuwa na timu ya taifa ya ufuatiliaji na tathmini kutoka kwa wawezeshaji wa mafunzo haya, itakayopitia baadhi ya shule baada ya miezi miwili ili kuona matokeo ya kile kilichofundishwa. Wanapokuja, wanataka kuona tofauti kati ya hali ya awali na baada ya mafunzo,” amesema Maiga.

Kwa upande wake, Vumilia Msukuma, ambaye alizungumza kwa niaba ya wawezeshaji wa mafunzo hayo, amewahimiza washiriki kuhakikisha wanatekeleza kwa vitendo yale waliyofundishwa kwa ajili ya manufaa ya watoto, hususan katika kupunguza changamoto za KKK na somo la Kiingereza mashuleni.

Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo,  Nashon Jonas, amesema mafunzo hayo yamempa mbinu mbalimbali za kukabiliana na changamoto ya KKK shuleni kwake, na ameahidi kuanzisha darasa maalum kwa ajili ya kuwashirikisha walimu wenzake maarifa aliyoyapata.

Naye Diana Nyumayo amesema kuwa mbinu zote alizojifunza katika kipindi hicho cha siku tatu atazitekeleza moja kwa moja darasani ili kuwasaidia wanafunzi kuondokana na changamoto ya KKK.

Matangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO ILIYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU January 08, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI February 17, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA February 21, 2024
  • MWALIKO WA ZABUNI KUPANGISHA ENEO KWAAJILI YA MGAHAWA March 08, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • WALIMU SHULE YA MSINGI KISUMA WATOA SHUKRANI KWA WADAU WALIOCHANGIA SARE NA VIFAA KWA WANAFUNZI

    June 05, 2025
  • MAFUNZO YA SIKU TATU YA KKK KWA WALIMU WA DARASA LA KWANZA NA LA PILI YAFIKIA TAMATI KASULU

    June 05, 2025
  • KASULU DC YAENDELEA KUWAJENGEA UWEZO WALIMU WA MADARASA YA AWALI

    June 03, 2025
  • VIONGOZI WA TAASISI ZA ELIMU NA IDARA YA AFYA KASULU WATAKIWA KUSIMAMIA USAFI WA MAZINGIRA

    June 02, 2025
  • Angalia Zote

Video

NAIBU WAZIRI OR-UTUMISHI NOV 2022
Video zaidi

KURASA ZA KARIBU

  • PlanRep_Web_Based
  • FFARS Online Manual
  • PlanRep Online Manual
  • Facility Financial Accounting and Reporting System (FFARS)
  • safari_Live
  • safaridemo
  • Dashibodi ya Ukusanyaji wa Mapato
  • UNICEF Dashboard
  • Kamusi Eng & Swa

TOVUTI ZINAZOHUSIANA

  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • TAMISEMI
  • BUNGE
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • ARIDHI
  • OPEN UNIVERSITY
  • PSPTB
  • AJIRA
  • HFR Dashboard
  • KIGOMA DC
  • NACTE
  • NECTA
  • eMrejesho

Kihesabu watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU

    Anuani ya Posta: S.L.P 97

    Simu ya Mezani: +255-028-2810339

    Simu: +255-028-2810339

    Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera Ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma
    • Wasiliana Nasi

Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.