Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akipokea Ramani ya Tanzania inayoonyesha Mikoa iliyopungua ugonjwa wa Malaria nchini kutoka kwa Mkurugenzi wa Ofisi ya takwimu Tanzania Dkt.Albina Chuwa.
Na.Andrew Mlama.
Waziri wa Afya Ustawi wa Jamii Jinsia Wazee na watoto Mh. Ummy Mwalimu, ameongoza maelfu ya wakazi katika maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yaliyofanyika leo katika Uwanja wa Umoja uliopo mjini Kasulu mkoani Kigoma.
“Katika kuhakikisha tunatokomeza ugonjwa wa Malaria, Wizara ya Afya kupitia Bohari kuu ya dawa (MSD) tumepokea na kusambaza vitendanishi vya Malaria (MRTD) Vipimo, 21,428,725, dawa za Mseto dozi 12,916,050 kwa ajili ya Malaria isiyo kali,sindano za kutibu malaria kali vichupa 1,668,464, vidonge vya SP 1,668,464 kwa ajili ya tiba kinga dhidi ya athari za malaria wakati wa ujauzito”alifafanua Mwalimu.
Alisisitiza kuwa, akina mama wanaonza kliniki ni lazima wapatiwe chandarua chenye dawa ya muda mrefu bure. Hii njia bora ya kujikinga na mbu waenezao malaria. Vile vile tunafanya kazi kwa kushirikiani na Serikali kupitia Wizara ya Afya kitengo cha kupamba na Malaria nchini ambao wamekuwa wakipuliza dawa yenye viatilifu kwenye maeneo yenye masalia ya mbu.
“Sisi kama Wizara, kazi yetu ni kuhakikisha hali ya ugonjwa wa malaria inapungua. Kwa sababu hiyo, tumekuwa na zoezi endelevu la kugawa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu kwa kila kaya hapa nchini. Vile vile, tunatumia vituo vya afya kuwafikia walengwa wakuu ambao ni akinamama wanaoenda kliniki na watoto wenye umri chini ya mwaka mmoja” alisema Mwalimu.
Amezitaka Halmashauri zote za Wilaya kuhakikisha zinaunda kamati zitakazohakikisha zinahamasisha usafi wa Mazingira ili kuondoa mazalia ya mbu na kutokomeza Malaria kabisa.
Naye Waziri wa Elimu na Ufundi Prof.Joyce Ndalichako alisema kuwa, atahakikisha Wanafunzi wanapambana na ugonjwa wa Malaria kwa kuweka Somo la afya katika shule za msingi na sekondari nchini.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emmanuel Maganga, amewataka wakazi wa mkoani hapa kuhakikisha wanatumia Vyandarua kwa matumizi lengwa badala ya kufugia kuku na kutumika kama nyenzo za uvuvi.
Kilele cha maadhimisho ya Malaria kimetamatishwa leo mjini Kasulu kikibeba kauli mbiu isemayo “NIKO TAYARI KUTOKOMEZA MALARIA WEWE JE?”
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.