Na Mwandishi Wetu
Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, mkoani Kigoma, leo Ijumaa Juni 20, 2025, imetoa mikopo yenye thamani ya shilingi 870,331,000 kwa vikundi 84 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kwa ajili ya robo ya tatu na ya nne ya mwaka wa fedha 2024/2025. Mikopo hiyo imetolewa kutoka 10% ya mapato ya ndani ya halmashauri kwa lengo la kuwawezesha wanufaika kuongeza mitaji ya shughuli zao za uzalishaji na kujikwamua kiuchumi. Kwa mujibu wa taarifa ya halmashauri, utoaji huo umefanya jumla ya mikopo iliyotolewa kwa mwaka huo wa fedha kufikia shilingi 1,363,491,000, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuunga mkono makundi maalum na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika Wilaya ya Kasulu.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.