Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma,Mhe. Kanali Isaac Mwakisu amesema kuwa katika kipindi cha miaka 61 ya Muungano wa Tanzania, Wilaya ya Kasulu imepiga hatua kubwa za maendeleo,ikonyesha mafanikio kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali mikubwa.
Akizungumza leo,Jumamosi Aprili 26,2025, wilayani humo wakati wa maadhimisho ya miaka 61 ya Muungano, Kanali Mwakisu ameeleza kuwa miradi hiyo inajumuisha ile ya maji,vituo vya afya,zahanati na hospitali,pamoja na ujenzi wa madarasa katika shule za msingi na sekondari,sambamba na kuanzishwa kwa shule mpya.
Amesisitiza kuwa mafanikio hayo yametokana na juhudi za marais wote waliooliongoza Taifa,kwa kubeba maono ya waasisi wa Muungano,na kuendelea kutekeleza miradi ya maendeleo kwa manufaa ya wananchi.
Aidha,Kanali Mwakisu ametangaza kuwa kuanzia Mei 1 hadi 7,2025, awamu ya pili ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura itaanza.Amehimiza wananchi kuhakikisha wanahakiki taarifa zao katika vituo walivyojiandikisha awali, ili kuwa tayari kwa chaguzi zijazo.
Pia,amewataka vijana kuhakikisha wanakuwa na vitambulisho vya Taifa ,akisisitiza kuwa fursa za ajira ziatapatikana kwa wingi wakati wa ujenzi wa kipande cha Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Tabora hadi Burundi,ambapo 84% ya utekelezaji wa mradi huo utafanyika wilayani Kasulu.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kasulu, Mbelwa Chidebwe, amewataka wanannchi kudumisha amani,umoja na mshikamano hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu,akisisitiza kuwa tofauti za kisiasa zisilete mafarakano,kwani maisha yataendelea hata baada ya uchaguzi.
Naye,Mratibu wa Mafunzo kutoka Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kasulu (FDC), Helena Shemweta,amesema kuwa Muungano ni jambo ambalo limendelea kuwa nguzo muhimu ya mshikamano,amani na maendeleo ya watanzania katika Nyanja mbalimbali za maisha.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.