Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma imepata fursa ya kuwajengea uwezo wataalam wake wa afya pamoja na kutoa huduma za kibingwa kwa wananchi kupitia Madaktari Bingwa wa Mama Samia.
Hayo yamebainishwa leo Juni 13,2024 na Dkt. Amani Mkemwa kwa niaba ya Mganga Mkuu wa hospitali ya wilaya hiyo alipozungumza na mwandishi wetu kuhusina na ujio wa madaktari hao.
Dkt Mkemwa ameeleza kuwa kupitia huduma za kibingwa zinazotolewa na madaktari hao wananchi wasiojiweza kiuchumi wameweza kupata huduma wakiwa katika maeneo yao kutokana na huduma za afya kusogezwa karibu.
"Zoezi hili kwetu ni kama fursa ndio maana wataalam wetu wa afya wanapata uzoefu kutoka kwa madaktari hawa ili wakiondoka wale wa kwetu watoe huduma zinazofanana na za kibingwa," amesema.
Mmoja wa madaktari hao bingwa wa Mama Samia, Daniel Gurisha amesema zoezi hilo limesaidia kuwapunguzia wananchi gharama kwa kupata huduma kwenye maeneo yao na si kwenda katika hospitali za rufaa za Kanda na taifa.
Gurisha ambaye ni Daktari Bingwa wa Usingizi na Ganzi ameongeza kuwa zoezi hilo limewajengea uwezo wataalam wa afya kitu kitakachisaidia utolewaji wa huduma zinazofanana na kibingwa itakapohitajika.
Kwa upande wake Mwananchi wa Kijiji cha Nyakitonto, Edward Nsuhuzwa amemshukuru Mhe.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwakumbuka wananchi wake na kupeleka huduma za afya za kibingwa karibu yao.
Ambapo amemuomba Mhe. Rais kuendelea kupeleka huduma hizo zaidi kwa wananchi kwa kuwa zinazosaidia kupunguza vifo.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.