Kamati ya fedha, uongozi na mipango ya halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, imeridhishwa na kasi ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika halmashaauri hiyo.
Hayo yamebainika wakati wa ziara ya kamati hiyo iliyofanyika mwishoni mwa mwezi Aprili.
Wakizungumza wakati wa ziara hiyo wajumbe wa kamati hiyo wamesema, kutokana na kasi ya kazi zinazofanyika katika miradi hiyo, wanayo matumaini kuwa miradi waliyoikagua, itakamilika katika muda unaotarajiwa.
Miongoni mwa miradi waliyoikagua wakati wa ziara hiyo, ni ujenzi wa makao makuu ya halmashauri, ujenzi wa wodi ya kulazwa wagonjwa wa magonjwa ya mlipuko, ujenzi wa nyumba za watumishi wa afya na ujenzi wa shule ya sekondari inayojengwa kwenye kijiji cha Kalela.
Wakati huo huo kamati ya fedha, uongozi na mipango ya halmashauri ya wilaya ya Kasulu, Jumatatu Mei 2 imefanya kikao chake cha kawaida kujadili agenda mbalimbali kwa masilahi na mustakabali wa halmashauri hiyo.
Picha ya juu ni wajumbe wa kamati ya fedha, uongozi na mipango wakiwa katika eneo la ujenzi wa makao makuu ya halmashauri.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.