Na Mwandishi Wetu
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu,Dkt.Semistatus H.Mashimba ametekeleza agizo la Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Phillip Mpango alilolitoa juzi Julai 12,2024 lililomtaka kujitambulisha na kusikiliza changamoto za wananchi wa Kata ya Nyakitonto yaliyopo makao makuu ya halmashauri.
Dkt.Mashimba ametekeleza agizo hilo jana Julai 13,2024 ambapo kupitia tukio hilo amekubaliana na wananchi kuanzishwa mpango kabambe wa matumizi bora ya ardhi ili kuzuia migogoro inayojitokeza baina ya wakulima,wafugaji pamoja na taasisi.
Amesema amekubaliana na wananchi kuanzishwa mpango huo kutokana na wilaya hiyo kuwa na changamoto kubwa ya uvamizi wa ardhi katika maeneo mbalimbali.
Tofauti na hayo pia amewaagiza watenda wa kata na maafisa mapato wa halmshauri hiyo kusimamia maagizo ya serikali yanayotaka kutowatoza ushuru wakulima wanaosafirisha mazao chini ya tani moja.
Katika hatua nyingine Dkt.Mashimba amewataka wananchi wanaoishi maeneo jirani na miradi ya maendeleo inapotekezwa kuisaidia serikali kwenye usimamizi wake ili inapokamilika iwe katika ubora unaotakiwa.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.