Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe ambaye ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Brigedia Jenerali Marco Gaguti akihutubia vijana waliohitimu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa Operesheni Mererani (Hawapo pichani) Kambi 825 KJ Mtabila Wilayani Kasulu.(Picha kwa hisani ya mlamamediablogspot.com)
Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Brigedia Jenerali Marco Gaguti amewataka vijana waliohitimu mafunzo ya Operesheni Mererani waondokane na mawazo ya kuajiriwa bali wajielekeze kwenye kujiajiri kutokana na ujuzi walioupata ili wakawe mfano bora katika jamii. Ameyasema hayo leo wakati akifunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana 798 katika kikosi cha 825 KJ kilichopo Mtabila wilayani Kasulu.
Amsema, mafunzo yasitumike tofauti na malengo kwani jamii inahitaji ulinzi mkubwa kutoka kwa vijana hao kwa kushirkiana na vyombo vya dola ili kutoa taarifa za uhalifu. Pia amewataka kuepuka vishawishi na kulinda Afya zao kwa kutotumia vilevi, kufanya zinaa na starehe nyingine hatarishi.
“Hongereni sana kwa kutimiza vigezo vinavyotakiwa, mmeonyesha utofauti kwani mmejengeka katika dhana ya JKT ambayo ni uhodari, uzalendo, utii na uaminifu. Hongereni pia kwa kazi nzuri mliyoifanya Kilimo kwanza kwa kuimarisha usalama na kutoa mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa wakulima” amesema Gaguti.
Amehitimisha kwa kuahidi kushirikiana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Mh. Yohana Mshita katika kutatua changamoto ya ukosefu wa Umeme pia kuhamisha Barabara inayopita kambini ili ipite nje ya eneo hilo.
Wakisoma risala, wahitimu hao wamemuomba Mkuu wa Wilaya kutatua changamoto ya ukosefu wa Umeme iliyopo kambini hapo pamoja na barabara kupita katikati ya kambi ya kikosi. Aidha, Wamefanikiwa kujenga nyumba ya Mkuu wa kikosi ikiwa ni sehemu ya kuonyesha uzalendo wao na bidii. Wameushukuru uongozi wa Serikali ya Rais. John Pombe Magufuli pamoja na kikosi kwa kazi nzuri zinazofanyika.
Hafla hiyo imehitimishwa kwa utoaji wa zawadi kwa vijana walioonyesha umahiri katika nyanja mbalimbali wakati wa mafunzo kambini hapo.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.