Shamba la bangi zaidi ya hekari moja iliyo kuwa imelimwa katika hifadhi ya pori la Akiba Makere Kusini lateketezwa.
Posted on: March 27th, 2017
Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilayani Kasulu,imeteketeza Shamba la bangi zaidi ya hekari moja iliyokuwa imelimwa katika hifadhi ya pori la Akiba Makere Kusini.
Miongoni mwa watuhumiwa waliokamatwa, wawili ni raia wa nchi jirani ya Burundi waliokuwa wakifanya kazi katika shamba hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Mkuu wa wilaya ya Kasulu ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Kanali Marko Gaguti wakati wa kuteketeza shamba hilo alisema:
"kumekuwa na tabia ya wakulima wengi kulima bhangi pembezoni mwa mji wakichanganya na mazao Mengine suala linalopelekea watoto wengi kuharibika na uhalifu kuongezeka".