Kwa mujibu wa sheria unaweza kupata cheti katika Wilaya uliyozaliwa au katika ofisi za Msajili Mkuu, Makao Makuu ya RITA katika jengo jipya la wakala la Rita Tower lililopo Mtaa wa Makunganya maeneo ya posta mpya mkabala na Club Bilcanas, Dar es Salaam.
Tafadhali fika katika ofisi zetu, utatakiwa
kujaza fomu BD 15
halafu utaambatisha kiambatishi kimoja kati ya hivi: kadi ya kliniki, cheti cha kupigia kura (2005), pasi ya kusafiria, cheti cha kumaliza elimu ya msingi au secondary (leaving certificate), cheti cha ubatizo. Kimoja wapo kati ya vilivyo tajwa hapo utakiambatanisha kwenye fomu yako utakayoijaza
halafu msajili atapitia maombi yako
yakiwa sawa utaandikishwa.
Je kama mtu hana Kimoja wapo kati ya vilivyo tajwa je inatakiwa afanye nini?
Nenda katika wilaya uliyozaliwa, chukua barua kutoka kwa afisa mtendaji kata wa sehemu uliyozaliwa ambayo ukiiwakilisha kwa msajili wa wilaya hiyo na msajili kujiridhisha utasajiliwa na kupata cheti. Karibu sana
Ghalama zikoje?
Tafadhali tuambie una umri gani na ulizaliwa wilaya gani, na kama una tangazo la kizazi ili tuweze kukutajia gharama ya cheti.
Ofisi ziko wapi?
Tuna ofisi kila wilaya ila makao makuu ya RITA yapo katika jengo jipya la wakala la Rita Tower lililopo Mtaa wa Makunganya maeneo ya posta mpya mkabala na Club Bilcanas, Dar es Salaam.
Ofisi ya RITA Kinondoni ipo jirani na Magomeni traffic light ukiwa unaenda Morocco. Utaona jengo limeandikwa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Kinondoni.
Masaa ya kazi:
siku za kazi ni kila siku kuanzia Jumatatu mpaka Ijumaa kuanzia saa 2.00 asubuhi mpaka saa 9.30 jioni.
B: UTARATIBU WA KUPATA LESENI YA BIASHARA
Leseni ya Biashara
Hiki ni kibali maalum cha Serikali kinachotolewa kwa mfanyabiashara yeyote anapotaka kufanya biashara hapa nchini. Sheria ya Leseni za Biashara Na. 25 ya 1972 – Kifungu cha 3(a) kimeweka bayana kuwa, Kibali hicho maalumu kinaitwa Leseni ya Biashara. Kwa hiyo basi, kufanya biashara yoyote bila kuwa na kibali hiki ni kosa la jinai.
Ili Mwombaji Apate Leseni Ya Biashara Anapaswa Kumbatanisha Nyaraka Zifuatazo:
· Nakala ya hati ya kuandikisha jina la Biashara au Kampuni (Photocopy of Certificate of Incorporation or Registration & Extract);
· “Memorandum, and Articles of Association” ambazo zitaonyesha kuwa Kampuni imeruhusiwa kisheria kufanya biashara inayoombwa, pamoja na majina ya wamiliki wa kampuni, hisa zao na utaifa wao;
· Uthibitisho wa uraia kwa kuwasilisha, nakala ya hati ya kusafiri nje ya nchi ya Tanzania au hati ya kusafiri katika nchi za Afrika Mashariki, cheti cha kuzaliwa au hati ya kiapo (Affidavit) kuonyesha kuwa ni Mtanzania, na kama mgeni alete hati ya kuishi nchini daraja la kwanza (Residence Permit Class A).
· Endapo wenye hisa wote wapo nje ya nchi itabidi maombi yaambatane na hati ya kiwakili (Power of Attorney) ya kumpa mamlaka raia wa Tanzania, raia wa kigeni mwenye hati ya kuishi nchini daraja “A” au hati ya kufanya kazi nchini daraja “B” zinazoainisha kuwa anasimamia kampuni husika.
· Nakala ya ushahidi wa maandishi kuwa ana mahali pa kufanyia biashara (lease agreement, Title deed, Certificate of occupancy, e.t.c);
· Hati ya kujiandikisha kama mlipa kodi (Tax Payer Identification Number - TIN).